Na.Faustine Gimu Galafoni,
Ikiwa leo Juni 25,2019 Bunge la Tanzania likiwa lina piga kura ya ndio au hapana ya kuipitisha au kutoipitisha bajeti kuu ya serikali,wabunge wamekuwa wakitoa michango na maoni mbalimbali kuhusu bajeti hiyo ambapo mbunge wa Rujiji Mohamed Mchengelwa ameishauri serikali kuongeza tozo kwenye Pombe na sigara.
Mhe.Mchengelwa amesema kuongeza tozo kwenye pombe na sigara itasaidia kulinda afya za watu kwani watapungua kunywa pombe na sigara kutokana na gharama kubwa ya bidhaa hizo ambazo sio muhimu kwa maisha ya binadamu kwani husababisha madhara kiafya pamoja ,uchumi kudumaa, migogoro kutokana na walevi kuwa na fujo zisizo za msingi.
Hivyo Mbunge huyo amesema serikali hutumia gharama kubwa katika matibabu kwa watu walioathirika na utumiaji wa pombe na sigara Mfano,TB, ili kupunguza gharama hizo na kuepusha madhara kwa watanzania ni wakati sasa umefika tozo za pombe na Sigara zikawa kubwa maradufu.
Katika hatua nyingine mbunge huyo ameishauri serikali kufanya tathmini ya Madhara ya Ukoloni uliotokea na kubainisha hasara na madhara ya ukoloni ili Tanzania ifungue kesi ya kimataifa dhidi ya nchini zilizokuwa makoloni ya Tanzania ambazo ni Ujerumani na Uingereza ili ziweze kuipa fidia Tanzania kwani baadhi ya nchi za Afrika zilishawahi kufanya hivyo na kulipwa.
Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya miezi ya hivi karibuni kuona clip ya video ya Bunge la Ujerumani ikishinikiza Taifa la Tanzania kusitisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa mto Rufiji wa Stieglers Gorge wakidai kuwa wao ni koloni la Tanzania.
Ikumbukwe kuwa mradi wa umeme wa Mto Rufiji Stieglers Gorge unagharimu dola za kimarekani Bilioni 2.9 na ukikamilika utazalisha Megawati 2,100 na hatua hiyo ya utekelezaji imekuja baada ya miaka 40 ya utafiti.
Social Plugin