Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE JAGUAR WA KENYA ABURUZWA MAHAKAMANI

Mbunge wa Starehe, nchini Kenya Charles Njagua maarufu Jaguar na amefikishwa mahakamani leo. Hata hivyo, ametupwa ndani hadi kesho mahakama itakapoamua iwapo ataachiliwa kwa dhamana.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) yaomba Mbunge huyo azuiliwe kwa siku 14 kwa uchochezi na kutoa vitisho dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni.

Hapo jana Mbunge huyo alikamtwa nje ya majengo ya Bunge kufuatia kauli zake za ‘kibaguzi' akiwataka wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wanaoendesha shughuli zao katika masoko mjini Nairobi na miji mingineyo kuondoka nchini humo ndani ya saa 24



Mbunge huyo analionekana katika video fupi ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii akizungumza na wafanyabiashara wa jijini humo na kuwaeleza kuwa hawatokubali watu wa nje waje kufanya biashara nchini mwao.


''Wakenya ni sharti wafanye biashara zao bila kushindana na watu kutoka mataifa mengine. Raia wa Pakistan wametawala biashara za kuuza magari nchini humu, Watanzania na Waganda wanatawala katika masoko yetu. Tunasema imetosha iwapo hawatarajeshwa nyumbani katika saa 24 tutawashika na kuwapiga na hatuogopi mtu yeyote,” alisisitiza mbunge huyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com