Mchezaji mwingine kutoka Brazil mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) amesaini mkataba wa miaka miwili na Mabingwa wa nchi.
Gerson Fraga Vieira ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson.
Pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo Grêmio amejiunga na klabu yetu akitokea ATK
Social Plugin