Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi-Mawasiliano TANAPA,Pascal Shelutete akieleza sababu za Tanapa kutoa tuzo kwa kampuni ya AngloGold Ashanti Ltd kutokana na mchango wake kwa shirika wa kutangaza Mlima Kilimanjaro pamoja na kuongeza pato la shirika.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi-Mawasiliano TANAPA,Pascal Shelutete akikabidhi tuzo maalumu kwa wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira na Geita,Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti wanaomiliki mgodi wa dhahabu wa Geita,Simn Shayo.
Wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira na Geita,Robert Gabriel wakimkabidhi tuzo maalumu iliyotolewa na TANAPA kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti wanaomiliki Mgodi wa dhahabu wa Geita,Simn Shayo.
Na Dixon Busagaga.Moshi
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeitunuku Kampuni ya AngloGold Ashanti Ltd tuzo maalumu kutokana na mchango wake wa kutangaza Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kupitia changamoto a kupanda mlima ikilenga kuchangisha fedha za Mapambano ya Virus vya Ukimwi lijulikanalo kama “Kili Challenge”
Tuzo hiyo imetolewa wakati wa hafla ya mapokezi ya washiriki 64 waliopanda mlima Kilimanjaro,wengine wakizunguka mlima huo kwa Baiskeli,hafla iliyofanyika katika lango la kushukia la Mweka na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikai wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira aliyekuwa mgeni rasmi.
Akimwakilisha Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi katika hafla hiyo,Kamishna Msaidizi Mwandamizi –Mawasiliano TANAPA,Pascal Shelutete alisema mbali na GGM kutumia Mlima Kilimanjaro kuchangisha fedha lakini pia kwa kiasi kikubwa wameshiriki katika kuutangaza Mlima huo.
"Niwashukuru wenzetu was Geita Gold Mining kwa kipindj Cha miaka 17 Sasa tangu walivyoanza zoezi hili,wamekuwa wakichangia pato la Shirika kupitia Mlima lakini pia kwa upande mwingine zoezi hili limekuwa likisaidia Sana kuutangaza Mlima Kilimanjaro ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu",alisema Shelutete.
"Tumeona ni vyema tunatambua mchango huo hasa ambapo tukio hili Lina fikisha miaka 17 kwa kutoa tuzo maalum kwa wenzetu hawa wa GGM ",aliongeza Shelutete.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira alisema mlima Kilimanjaro ni dhamana iliyotolewa na Mungu kwa watanzania hivyo serikali wajibu wake mkubwa ni kuhakikisha kwamba unaendelea kubaki salama na kuenziwa.
“Sisi watu kama serikali ni kuhakikisha kwamba Mlima Kilimanjaro unaendelea kubaki na kuenziwa ili uendelee kufaidisha nchi yetu na Dunia kwa ujumla na katika kuhakikisha hilo linatekelezeka tumeweka utaratibu maalumu wa kuhakikisha hauchafuliwi wala kuharibiwa kwa namna yoyote ile.”alisema Dkt Mghwira.
Dkt Mghwira alitumia nafasi hiyo kuwahimiza Serikali za wilaya zinazopakana na hifadhi ya taifa ya Mllima Kilimanjaro pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kukaa kwa pamoja kumaliza migogoro baina ya wananchi na hifadhi hiyo.
“Naomba kuhimiza kwa Serikali za wilaya pamoja na TANAPA kupitia KINAPA ya kwamba Migogoro yote inayohusu eneo la Mlima imalizwe,kuna migogoro ya Half Mile, inazungumzwa kila wakati na ni kama haiishi”,alisema Dkt Mghwira.
Aidha Dkt Mghwira aliwaomba wageni kutoka nje ya nchi kutoingilia masuala yanayohusu Mlima Kilimanjaro na badala yake watumie muda wao kuijifunza kutoka kwa watanzania kwani wao ndio wenye kuufahamu vizuri mlima huo.
“Niombe pia wageni ambao wanakuja kwetu hasa wale ambao wanakuja kwa shughuli za kijamii wajifunze kutoka kwetu ,wasituingilie sana kwenye eneo hili ,….hapa na pale tumekutana kila wakati na mazingira ya wageni kujiingiza mno kwenye masuala ya mlima.”alisema Dkt Mghwira .
“Wamekuwa wakijiingiza katika shughuli zinazofanyika hapa na kuteletea utata mgumu ,kwa sababu tunavyoshughulika na wageni wa nje ya nchi mahusiano yake yanakuwa tofauti kidogo na namna ya kufanya maamuzi”aliongeza Dkt Mgwira.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti kupitia mgodi wa Dhahabu Wa Geita,Simon Shayo alisema zadi ya Bil 13 zimekusanywa katika kampeni hiyo tangu ianze na kuungwa mkono na zaidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali 40.
“Tunafurahi kweli na tunashukuru kwa washirika wetu wote na tutaendelea kushirikiana kufanya kila liwezekanalo na kwa ambao pia wangependa kujiunga katika vita hivi hii inamaanisha wakihamsika wapandaji zaidi itasababisha watu binafsi na jamii zaidi kuunga mkono na mpango wa Kili Challenge”,alisema Shayo.
Shayo aliwashukuru wafadhili wa changamoto hiyo na wote walishiriki kupanda na kwamba jitihada walizoonesha ni muhimu katika kuchochea tukio hilo wakiwemo waendesha baiskeli ambao waliamua kuweka roho zao juu ili kuhakikisha Tanzania kupitia Kili Challenge inafikia sifuri 3 mwaka 2030.