Solomon Letato(30) mkazi wa Loliondo anashikiliwa na Jeshi la Polisi akihusishwa na matukio ya ujambazi baada ya kukutwa darasani na silaha ya AK-47 ikiwa na risasi 5 hapo jana.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani wa Arusha, Jonathan Shanna amesema kuwa mtuhuhumiwa huyo ambaye pia ni mwalimu aliyeajiriwa na serikali, alikamatwa katika kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro akituhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuingiza silaha za moto kutoka nchi jirani.
Pia Mwalimu huyo anatuhumiwa kujihusisha na kufanya biashara haramu ya nyara za serikali yakiwemo meno ya tembo na pembe za faru.
Wakati huo huo katika Kijiji cha Mbukeni, kata ya Arash wilayani Loliondo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK 47 iliyokuwa imetelekezwa katika Kijiji cha Embukeni kufuatia msako mkali wa jeshi la polisi unaoendelea wilayani humo.
Social Plugin