Mwanaume, aliyejihami kwa kishu asiyefahamika jina kabila wala makazi yake umri kati ya miaka 28 - 29 ameuawa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kukutwa akiiba bidhaa za duka kwenye duka la Bertha John (28), mkazi wa kijiji cha Nyashimbi, kata ya Puni, Tarafa ya Itwangi, wilaya ya Shinyanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Mei 30,2019 ya saa tano usiku kijiji cha Nyashimbi wilaya ya Shinyanga.
“Chanzo cha tukio hilo ni Marehemu kukutwa na mmiliki wa duka akiiba ambapo alipiga kelele za kuomba msaada na watu walijitokeza kutaka kumkamata marehemu, ndipo marehemu alipochomoa kisu alichokuwa nacho na kumjeruhi kiganja cha mkono wa kulia Thomas Selemani(30)”,ameeleza.
“Kutokana na hali hiyo wananchi hao walichukua uamuzi wa kumuua na kumchoma moto shambani kwa Shigila Kitebbi ( 70), Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari wa Serikali na kukabidhiwa kwa Viongozi wa Kijiji kwa taratibu za mazishi”,ameongeza Kamanda Abwao.
Amesema juhudi za kuwakamata waliohusika na tukio hilo zinaendelea.
Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin