Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye amezungumzia kuhusiana na kutajwa katika ujumbe uliochapishwa kwenye akaunti ya kijamii ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe.
Kupitia ukurasa wa twitter wa Zitto umechapishwa ujumbe unaodai kuwa kiongozi huyo wa ACT- Wazalendo ameunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano na kuwataka viongozi wengine wa upinzani kuipongeza serikali na sio kukosoa kila kitu.
Nape ameandikwa kuwa, "Nimeona tweets zinazodaiwa kuwa za Ndugu Zitto zikinitaja, amekakanusha sio zake. Kilichonishangaza ni uwezo mdogo wa kufikiri wa wadukuaji! Mnanyimwa usingizi na nini?? Hamuwezi kuendelea na maisha msiponitaja!", amemalizia kwa kucheka.
Moja ya ujumbe uliochapishwa ambao Zitto mwenyewe pamoja na chama chake wamekanusha ujumbe huo umesema kuwa, "Wapo ambao najua wataniita majina mengi ya ajabu kwa maamuzi yangu haya kama jinsi ambavyo wamekuwa wakimshambulia ndugu yangu Nape Nnauye kwa kutokuwa na misimamo thabiti lakini nataka niwaambie huo ndio msimamo wangu na sitaki kuyumbishwa kwani hata Wanakigoma wamefaidika".
Taarifa ya chama cha ACT-Wazalendo iliyotolewa na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi imesema kuwa taarifa zinazowekwa hivi sasa kwenye akaunti ya Twitter ya Kiongozi wa Chama hicho Ndugu Zitto Kabwe si zake kwani simu na laptop yake vipo mikononi mwa Jeshi la Polisi.
Social Plugin