Mchungaji mmoja nchini Nigeria, Peter Adegoke Adewuyi, wa kanisa la 'The Methodist Church' amekatwa baada ya madai kuwa alijiteka nyara na kuanza kuitisha washirika wa kanisa lake kitita cha fedha ili aachiliwe huru.
Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa ameripotiwa kutekwa nyara akielekea Ado Ekiti JUmapili, Juni 9,2019.
Habari nchini humo zilisema kuwa mhubiri huyo pamoja na rafiki yake walijiteka nyara ndani ya hoteli moja ambapo waliwapigia washirika simu na kutaka fedha zitumwe la sivyo mchungaji wao auawe.
'Watekaji nyara' hao walisema mchungaji angeuawa kufikia Alhamisi, Juni 13,2019 iwapo hawatapokea pesa kumkomboa.
Hata hivyo, makachero walifuatilia simu yake na kuwapata kwenye hoteli wakipunga unyunyu.
"Polisi walifuatilia mazungumzo ya simu na kuwapata wawili hao kwenye hoteli," polisi walisema.
Wawili hao kwa sasa wanazuiliwa huku uchunguzi ukikamilishwa huku wakitazamiwa kufikishwa kortini.
Social Plugin