POLISI PWANI YAWASAKA WATU WANNE WANAODAIWA KUPORA PIKIPIKI


Mwamvua Mwinyi,Kibaha
JESHI la polisi mkoani Pwani,linawasaka watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao wanadaiwa kupora pikipiki eneo la Kidimu kata ya Pangani Kibaha Mjini .

Aidha jeshi hilo limewatahadhalisha madereva bodaboda kuacha kuamini abiria wanaokodisha pikipiki zao kwenda nje ya mji kwani sio wote ni abiria wema.

Akielezea juu ya tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa alisema kuwa ,watu hao wakiwa Kidimu kata ya Pangani,barabara ya Kibaha kupitia Mapinga kuelekea Bagamoyo walipora pikipiki ambayo mmoja wao aliikodi kutokea Mwanalugali Kibaha.

Wakiwa Kidimu walitumia gari Toyota IST rangi ya silver yenye namba za usajili T.355 DMA ambapo mmoja wao alikimbilia Mwanalugali na kukodisha pikipiki yenye namba MC 401 CDW aina ya hajoue ya bwana Amani Ambele.

Wankyo, anasema baada ya hapo jambazi huyo aliomba apelekwe Kidimu kwa sh.3,000 ambako Kidimu kulikuwa tayari na wenzie watatu wakiwa na gari yenyr namba T 355 DMA .

“Walipofika hapo abiria ambae ni anaedaiwa kuwa ni jambazi alimfunga kitambaa cheusi usoni na kumuingiza katika gari na kisha kuondoka na pikipiki”

“Bahati nzuri madereva boda wengine wa mjini Kibaha walipata taarifa na kuanza kulifukuzia gari hilo na walipolipata walilichoma moto na liliteketea huku majambazi hayo yakifanikiwa kukimbia”alifafanua Wankyo.

Wankyo alielezea kuwa, baada ya madereva bodaboda hao kuteketeza gari hilo kwa moto walitoa plate namba ,kadi ya gari na bima na kuwasilisha polisi.

Wakati huo huo kamanda huyo alisema jeshi hilo limejipanga kufanya misako ili kulinda raia na mali zao wakati wa sikukuu ya iddi el fitri.

Hata hivyo Wankyo,aliwaasa madereva kuacha kukiuka sheria za usalama barabarani wakati wa sikukuuu na kuacha kutumia vileo wakiwa wanaendesha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post