Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), Michael Pius Nyagoga.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa, utenguzi huo umeanza leo Juni 17, 2019.
Aidha kutokana na uamuzi huo, Rais Magufuli amemteua Wakili Julius B. Kalolo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA), kuanzia leo Juni 17, 2019.
Social Plugin