Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini imedhamiria kufikisha umeme katika vijiji vyote visivyo na umeme nchini ifikapo Juni 2021.
Hayo yameelezwa bungeni jana Juni 18, na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Monduli Julius Laizer (CCM) aliyetaka alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka umeme katika shule ya Sekondari Oldonyolengai ambapo lami imefika toka mwaka 2015 lakini mpaka sasa hakuna umeme.
Akijibu swali hilo Subira alisema kulingana na mpango wa kupeleka umeme katika vijiji 64 wilayani Monduli, vijiji 16 vilishapatiwa umeme kupitia awamu ya pili ya miradi ya kusambaza umeme vijijini (REA-11), vikiwemo vijiji vya Arkatani na Mti.
Alisema kazi za mradi zinahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilometa 48.75 na njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 0.4 yenye urefu wa kilometa 40.
Social Plugin