Serikali imekiri ‘udhaifu’ katika utekelezaji wa vitambulisho vya wajasiriamali na imesema itatoa waraka utakaoelekeza ni nani anatakiwa kutozwa kodi na nani anatakiwa kupata vitambulisho.
Hayo yameelezewa leo Jumanne Juni 25, 2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge.
Katika swali lake Chenge amesema ni kwa nini Serikali isitoe waraka kueleza kodi zote zilizofutwa na Bunge la Tanzania pamoja na maelekezo ya wanaostahili kupewa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ili kuwe na usawa nchi nzima.
Akijibu swali hilo naibu Waziri wa Tamisemi, Waitara amesema, “Waraka kuhusu kukodi zote zilizofutwa ni jambo ambalo tumelipokea na tutautoa huo waraka na kugawa maeneo mbalimbali.”
“Kuhusu vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kuanzia Julai 2019 tutatoa maelekezo ya nani anayepaswa kuwa na vitambulisho hivi.”
==>>Tazama hapo chini
Social Plugin