Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Kamati ya bunge ya bajeti imeishauri serikali kuhakikisha inaunganisha taasisi zote zenye majukumu yanayofanana ikiwa ni pamoja na TBS, OSHA, TFDA na Fire ili kuondoa kero na usumbufu kwa wafanyabiashara
Hayo yamesemwa Juni 17,2019 bungeni jijini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Bajeti George Simbachawene wakati akiwasilisha taarifa ya kamati ya bajeti kuhusu hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 na mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 pamoja na tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2018/20 na mapendekezo ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2019/20.
Mhe.Simbachawene amesema ilikurahisisha utekelezaji katika maeneo mbalimbali ni vyema kuunganisha taasisi hizo ili kuondoa kero na usumbufu unaojitokeza pindi taasisi hizo zinapotembelea na kufanya ukaguzi kwenye viwanda mbalimbali hapa nchini.
Aidha,Mhe.Simbachawene amesema pamoja na nchi yetu kuwa na Rasilimali kubwa ya mifugo na samaki bado haijaweza kunufaisha wananchi na taifa kwa ujumla hivyo ni wakati umefika kuacha kujipongeza kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo na badala yake kujielekeza kuongeza kasi ya kutumia Baraka hizo kwa kunufaisha watu wa Taifa la Tanzania Pamoja na kunufaisha sekta ya kilimo.
Kuhusu suala la Madini Mhe.Simbachawene amesema bado kuna tatizo kwa baadhi ya wafanyabiashara kutorosha dhahabu kwenda nje ya nchi kwani kiwango cha kilo 600 za dhahabu zilizouzwa katika soko la Geita ni kidogo.
Wakichangia maoni juu ya taarifa ya bajeti kuu ya serikali baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Sumve Kwimba Richard Ndassa wamesema kuna haja kubwa ya serikali kuangalia upya sekta ya kilimo hususan Soko ili kuinua wanyonge.
Social Plugin