Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imeandaa kiasi cha Sh.Bilioni 82,milioni 975 laki 9,na 94 elfu ,na mia 148 kwa ajili ya kuendesha uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2019.
Hayo yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Ofisi ya Rais,TAMISEMI,Mwita Waitara wakati akijibu swali la mbunge wa Mtambile Masoud Salim aliyehoji ,mwaka 2019 utafanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria ,je,serikali ina mkakati gani unaoendelea katika maandalizi ya mchakato wa Uchaguzi huo.
Katika Majibu yake Naibu waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe.Mwita Waitara amesema katika kuhakikisha uchaguzi waserikali za mitaa unafanyika kwa ufanisi ,serikali imekamilisha maandalizi ya kanuni hizo zilizotangazwa kwenye gazeti la serikali la tarehe 26/April/2019 tangazo Na.371,tangazo Na.372 , tangazo Na.373, na tangazo 374.
Hivyo Naibu Waziri Waitara amesema ,serikali imehakiki maeneo ya Utawala na kufanya mafunzo na mikutano kwa wadau wa uchaguzi ambapo serikali inaendelea na maandalizi ya ununuzi ya ununuzi wa vifaa vya uchaguzi na imetenga kiasi cha Sh.Bilioni 82,milioni 975,laki 9,94 elfu ,na 148 kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huo.
Social Plugin