Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James amezindua rasmi Kampeni ya ‘Shinyanga ya Kijani’,mkakati unaolenga kuwaandaa vijana wa CCM kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nchini utakaofanyika mwishoni mwaka 2019.
Kampeni hiyo kabambe imezinduliwa leo Jumatano,Juni 19,2019 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.
Akizindua Kampeni hiyo,Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James amesema Operesheni ya Kimkakati inayojulikana kwa jina la Mkakati wa kijani kwa upande wa mkoa wa Shinyanga itakuwa ni ‘Shinyanga ya Kijani.
“Huu ni mkakati wa kuwaandaa vijana wanachama wa CCM kote nchini kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nchini,kwa hiyo vijana wote wanaandaliwa kwa maana ya kuwaarifu kwamba mwaka huu uchaguzi utakuwepo”,alisema.
Alieleza kuwa mkakati huo unalenga kuwataarifu kuwa vijana wanalo jukumu la kujiandikisha katika madaftari ya wapiga kura kwenye maeneo yao na kujitokeza kugombea na kuwapigia kura wale watakaogombea pamoja na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na sheria za uchaguzi zinazingatiwa ili uchaguzi wetu uwe ni wa amani.
“Leo nimepata heshima ya kuzindua mkakati huu katika mkoa wa Shinyanga, imani yangu ni kwamba vijana leo tunawatangazieni kwamba uchaguzi mwaka huu upo,lakini nyinyi kama wananchi wengine mnayo fursa ya kugombea sawa na wengine,ili mpate haki hiyo lazima mjiandikishe ili mpate uhalali wa kuwa wananchi wakazi kwenye maeneo utakapofanyika uchaguzi”,alifafanua.
“Vijana mnalo jukumu la kushirikiana na chama chetu kuhakikisha wagombea wa chama chetu wanashinda uchaguzi wa serikali za mitaa,hiyo ni kazi ambayo tumekuja kuambizana leo na kuizindua rasmi katika mkoa wetu wa Shinyanga”,aliongeza James.
Aidha aliwataka vijana walioaminiwa na kupewa nafasi za uongozi watambue kuwa kuwa wameaminiwa kwa maslahi ya umma hivyo watumike kwa maslahi ya umma huku akiwataka vijana wanaopewa madaraka na kujifanya siagi na kuyeyuka zama zao zinahesabika akidai hakuna cheo kinachodumu.
“Tunahitaji kuwa wamoja,kushikana na kufanya kazi,MwanaCCM popote alipo ana jukumu la kuendelea kukijenga chama,kuwatumikia watanzania wenzetu kwa hali na mali ili mwisho wa siku ustawi wa Watanzania na taifa kwa ujumla viweze kupatikana na niwakumbushe tu kazi ya kuimarisha chama inaendelea kote nchini”,alisema.
Katika hatua nyingine alisema jukumu la vijana wa UVCCM ni kuwalinda viongozi wa CCM na kulinda chama dhidi ya maadui nje na wa ndani ya chama /wasaliti ndani ya chama kwa sababu siyo watu wote wanaoitwa viongozi wa CCM wanania njema na CCM wengine ni vibaraka wanaotumika kuidhoofisha CCM.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alieleza kuwa vijana wa CCM mkoani humo wapo imara na kwamba watahakikisha kuwa CCM inapata ushindi kila eneo na kwamba serikali itahakikisha kuwa Demokrasia inazingatiwa ili uchaguzi uwe huru na wa haki.
Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP),alisihi vijana kuwa na nidhamu na wavumilivu na kuwataka wanaCCM kupendana na kushirikiana huku akisisitiza kuwa CCM itashinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.
“Mwaka huu tutatimiza miaka 20 tangu baba wa taifa,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere afariki dunia,nataka niwaombe Jumuiya ya Vijana tujiandae kikamilifu kufikia mwezi Oktoba,na mimi nitatoa ushirikiano wote tushangilie maisha aliyoishi Baba wa taifa,yapo mambo matatu aliyapigania ambayo ni umaskini,maradhi na ujinga hao maadui bado tunao,naomba tuendelee kupigana na maadui hawa”,alisema Masele.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akivishwa skafu alipowasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani leo Juni 19,2019 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akipokelewa na vijana wa CCM alipowasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James (katikati) akiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa kuelekea katika Ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye pia Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP).Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCMMwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCMMwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akimkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James azungumze na viongozi mbalimbali wa CCM katika kikao cha ndani .Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM katika kikao cha ndani kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM katika kikao cha ndani kabla ya kuelekea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akizungumza katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akizungumza katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye pia Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (katikati) na Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Meza kuu wakiwa uwanjani.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP).
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akicheza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akishikana mkono na Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga,Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko (kulia) wakiteta jambo.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akiimba pamoja na Msanii Beka Boy (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Msanii Beka Boy akitoa burudani.
Wanachama wa CCM wakicheza na kupiga picha wakati wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele wakiwa jukwaani wakicheza wakati wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akiimba wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Diwani kutoka Nzega,ambaye pia ni Msanii wa nyimbo za Asili,Madebe Jinasa (katikati) akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Vijana wa halmashauri ya Shinyanga wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage.
Kikundi cha Hamasa kutoka Salawe halmashauri ya Shinyanga kikitoa burudani.
Wanachama wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Wanachama wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Wanachama wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Makada wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Wanachama wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Burudani ikiendelea kutolewa.
Wanachama wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Wanachama wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Wanachama wa CCM wakiwa eneo la tukio.
Burudani ikiendelea kutolewa uwanjani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akifurahia burudani kwa kupiga makofi.
Burudani ikiendelea.
Wanachama wa CCM wakiwa uwanjani.
Viongozi wa UWT mkoa wa Mwanza wakijitambulisha.
Viongozi wa Vijana kutoka mikoa mbalimbali wakijitambulisha.
Viongozi wa Vijana mkoa wa Shinyanga wakijitambulisha.
Viongozi wa vijana kutoka mikoa mbalimbali wakijitambulisha.
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani
Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani,wengine ni madiwani wa CCM mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu Haula Kachwamba akiwasalimia wanaCCM.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akikabidhi viakisi mwanga kwa waendesha bodaboda baada ya kuzindua kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akikabidhi viakisi mwanga kwa waendesha bodaboda baada ya kuzindua kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Zoezi la kugawa vyeti kwa watu/wadau wanaoshirikiana na CCM likiendelea.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akikabidhi jezi kwa vijana baada ya kuzindua kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Vijana wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza na viongozi wa CCM na mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akikabidhi jezi kwa vijana baada ya kuzindua kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin