Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam imeendelea kukisuka kikosi chake baada ya hii leo kumuongezea mkataba mchezaji wake nyota Raia wa Zambia Clatous Chota Chama.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambao kwa sasa katika kipindi hiki cha usajili imekuwa ikitambulisha wachezaji ambao imewasajili kuelekea msimu mpya wa mashindano 2019/2020.
Mfungaji huyo wa magoli ya mwisho ambayo yaliipeleka Simba kwenye hatua ya makundi na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Clatous Chota Chama (Triple C) bado yupo sana Msimbazi.
Mwamba wa Lusaka ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2018/19 baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Social Plugin