Klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga ambayo msimu ujao itashiriki katika ligi daraja la kwanza Tanzania Bara imetangaza nafasi za kazi kwa Kocha mkuu na Kocha msaidizi, ili kuboresha kikosi chake katika harakati za kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara.
Pia timu hiyo yenye maskani yake katika Viunga vya mji wa Shinyanga imetangaza kupokea wachezaji waliowahi kucheza ligi kuu Soka Tanzania Bara pamoja na wale ambao watatolewa kwa mkopo kutoka vilabu vya ligi kuu soka Tanzania Bara.
Social Plugin