Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMUUA MWANAYE KISHA KUMPIKA KAMA SUPU GEITA

Picha haihusiani na tukio

Katika hali inayositaajabisha na kuacha maswali mengi, mwanamke mmoja mkazi wa Kitongoji cha CCM,Kijiji cha Buligi Kata ya Senga Wilayani Geita, Happiness Shadrack (36), anayedaiwa ni mgonjwa wa akili, amemuua mwanaye wa kumzaa, Martha Yakobo (1), kwa kumkatakata vipande vidogovidogo kisha kumuweka ndani ya sufuria na baadaye kumpika kama kitoweo/supu.



  • Tukio hilo limetokea jana Ijumaa 7majira ya saa saba za mchana,muda mfupi baada ya mtoto aliyeuawa kupelekwa kulazwa kwenye chumba cha bibi yake, kama dada wa marehemu anavyosimulia ambaye amedai kuwa alikwenda kumlaza ndani na yeye kwenda kucheza nje, baada ya muda mfupi alimuona mama yake akiwasha jiko na kudai kuwa alikuwa akichemsha maji.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Kamishina msaidizi wa polisi Dismas Kisusi akithibitisha kwa njia ya simu kuwepo kwa tukio hilo amesema kuwa tayari mhusika amefikishwa kituo cha polisi na upelelezi unaendelea.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com