Imeripotiwa kuwa mtu mmoja nchini Kenya amepatwa na ugonjwa wa Ebola na tayari amelazwa katika Hospitali ya Kericho,nchini humo.
Taarifa za awali kutoka kwa Maafisa wa afya katika Kaunti ya Kericho wamesema kuwa, Mgonjwa huyo siku chache zilizopita alisafiri kutoka Malaba eneo la mpaka kati ya Kenya na Uganda.
Tayari Sampuli za damu za mgonjwa huyo zimechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya uchunguzi zaidi, kujua kama kweli ameathirika na virusi vya Ebola.
Kwa upande mwingine, Idara ya huduma za afya na serikali ya kaunti ya Kericho imesema inafuatilia kwa karibu suala hili na kuwahakikishia wananchi kuwa hatua madhubuti zinafuatwa kuhakikisha usalama wa kiafya kwa wengine.
Hili linakuwa ni tukio la pili kwa nchi za Afrika Mashariki kukumbwa na kisa cha mgonjwa wa Ebola, Baada ya wiki iliyopita kupatikana kwa mgonjwa mmoja nchini Uganda.
Social Plugin