Timu yetu ya Tanzania, Stars leo Jumapili June 23 itachuana na Senegal katika mchezo wa Fainali za Afcon, mechi itakayopigwa saa 2 usiku kwa saa za nyumbani (Tanzania).
Nahodha wa Taifa Satars, Mbwana Samatta amesema kamwe hawatokubali kufungwa kirahisi katika mchezo huo.
Samatta amesema anajua wanaenda kucheza na timu kubwa yenye wachezaji wanaotazamwa kila wikiendi katika ligi bora lakini hilo haliwatishi wao kupambana katika mchezo huo.
"Tunajua kwamba wapinzani wetu ni wazuri na tunawaheshimu, hatuendi kuwashangaa zaidi na sisi tunaenda kupambana nao na ndio maana tumejiandaa kwa muda mrefu kuweza kupambana," amesema.
Ameongeza anaamini mchezo huo mpaka dakika ya mwisho kila timu ina uwezo wa kupata matokeo uwanjani.
Social Plugin