Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : TCRA YAKUTANA NA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imeendesha mkutano wa wadau wa wa sekta ya mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kupokea maoni,mapendekezo na kusikiliza kero zinazohusu utendaji wa TCRA.

Mkutano huo wa siku moja umefanyika leo Juni 13,katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza na kukutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watoa maudhui kupitia TV,Radio,mitandao,mafundi simu,polisi,wauzaji na wasambazaji wa vifaa vya mawasiliano na wadau wengine.

Akizungumza wakati wa mkutano huo,Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo aliyataja baadhi ya majukumu ya TCRA kuwa ni kuimarisha ustawi wa Watanzania kupitia ukuzaji wa ushindani katika sekta ya mawasiliano wenye kuleta uchumi fanisi,kulinda maslahi ya watumiaji wa taarifa mbalimbali za mawasiliano.

Mhandisi Mihayo alisema jukumu jingine ni kusimamia upatikanaji wa huduma zinazokidhi viwango na vigezo na masharti ya usambazaji wa bidhaa na huduma za mawasiliano,kudhibiti tozo na viwango vinavyohusiana na huduma za mawasiliano,kusimamia utendaji kazi wa sekta ya mawasiliano ukilinganisha na kiwango cha utekelezaji uliowekwa.

Katika hatua nyingine alisema hadi kufikia Juni 10,2019 kumekuwepo na ongezeko kubwa katika eneo la simu za viganjani,huduma za intaneti,vituo vya redio ambapo sasa kuna makampuni sita yanayotoa huduma za simu na internet na makampuni manne yanayotoa huduma za internet pekee.

“Pia tuna vituo 38 vya utangazaji wa redio,vituo viwili vya utangazaji wa televisheni wanaorusha matangazo yao kupitia MUX operators,makampuni 24 ya utangazaji wa televisheni kwa kutumia teknolojia ya Cable na makampuni/taasisi 32 zinazotumia simu za upepo na watoa huduma 373 wanaojihusisha na biashara ya kuagiza,kusambaza na kuuza vifaa vya mawasiliano",alifafanua.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa wa sekta ya mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kupokea maoni,mapendekezo na kusikiliza kero zinazohusu utendaji wa TCRA.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akifungua mkutano wa wadau wa wa sekta ya mawasiliano Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akifungua mkutano wa wadau wa wa sekta ya mawasiliano Kanda ya Ziwa.
Wadau wa wa sekta ya mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com