Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI


Chelsea inapania kumuajiri kocha wa Derby Frank Lampard, kama maneja wake mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu kufikia mwisho wa wiki hii. (Standard)

Manchester United wamekubali kulipa ada ya pauni milioni 55 kumsajili mlinzi wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21. (Record)

Hata hivyo madai hayo yamekanushwa huku vilavu hivyo vikiendelea kushauriana kuhusu usajili wa kiungo huyo. (Mail)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amekuwa akitafuta nyumba mjini Barcelona,licha ya tetesi kuibuka kuwa nyota huyo wa Kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 anajiandaa kurejea Nou Camp. (Sport)Neymar

Bayern Munich wanajiandaa kujiunga na Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Rodri, 22, kutoka Atletico Madrid. (AS - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Brazil Jorginho yuko tayari kuondoka Chelsea na kwenda kujiunga na Maurizio Sarri katika klabu ya Juventus mwaka mmoja baada ya kusajiliwa na Napoli kwa kiasi cha pauni milioni 50. (Mirror)

Inter Milan na Atletico Madrid wanataka kusajili beki wa England anayechezea klabu ya Southampton Ryan Bertrand, 29. (Mail)

Juventus wanaamini wataipiku Real Madrid katika usajili wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mirror)Paul Pogba

Arsenal inapania kusaini beki wa Celtic raia wa Uskochi Kieran Tierney, 22, msimu ujao. (Mail)

Sporting Lisbon wanashauriana na Liverpool kuhusu usajili wa winga wa Ureno wa miaka 19, Rafael Camacho. (Standard)

Norwich wanamatumaini ya kumnunua beki wa England Max Aarons, 19, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Manchester United. (Telegraph)

West Ham wameifahamisha Manchester United na Manchester City kuwa hawana mpango wa kumuuza nyota wa Kimataifa wa England anaecheza safu ya kati Declan Rice, 20, msimu huu wa joto. (Sky Sports)Declan Rice

Arsenal wanajianda kuweka dau la kumnunua winga wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai, 18. (Football Insider)

Kipa Tom Heaton amekataa ofa ya kandarasi mpya aliyopewa na Burnley.

Kipa huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 33 ataingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake wa sasa katika uwanja waTurf Moor mwezi ujao. (Guardian)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com