Barcelona inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann kwa dau la £107m baada ya kifungu cha sheria cha uhamisho wake kuanza kufanya kazi tarehe mosi mwezi Julai (Telegraph)
Tottenham inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Tanguy Ndombele, 22, kwa dau litakalovunja rekodi £60m.
Ndombele aliichezea Lyon mechi 34 ,msimu uliopita huku ikifuzu katika mashindano ya ligi ya mabingwa baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu ya jedwali la ligi ya daraja la kwanza.. (Sun)
Spurs pia inakaribia kumsaini winga wa klabu ya Leeds United Jack Clarke 18, kwa dau la £8.5m. Clarke aliichezea klabu hiyo mara 22 msimu wa 2018-19. (Sky Sports)
Manchester United wanataka kumsaini mshambuliaji wa Sevilla na Ufaransa Wissam Ben Yedder, 28, na wataathiri kifungu cha sheria cha uhamisho wake cha £35.8m. (ABC de Sevilla)
Manchester United ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa ,15, Mathis Rayan Cherki anayeichezea klabu ya Lyon na ambaye anazivutia klabu kama vile Real Madrid, Juventus, Barcelona na Bayern Munich. (Telegraph)
Mlinda lango wa Liverpool na Ubelgiji Simon Mignolet, 31, ananyatiwa na klabu ya Crystal Palace. Mwewe hao wa Uingereza wameandaa dau la £8m kumnunua Mignolet, ambaye amesalia na kandarasi ya miaka miwili .. (Evening Standard)
Hatahivyo klabu hiyo ya Anfield haiko tayari kumuuza Mignolet kwenda Palace to Palace na itamuachilia kipa huyo iwapo kitita hicho kitakubalika. (ESPN)
Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, ambaye alifunga katika ushindi wa Liverpool dhidi ya Tottenham katika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya anasakwa na klabu ya Real Betis, huku klabu hiyo ya Uhispania ikiandaa dau la £10m kumnunua mchezaji huyo wa Ubelgiji . (BeIn Sports - in French)
Mshambuliaji wa West Ham na Mexico Javier Hernandez, 31,ana mipango ya kuondoka na kuelekea Uhispania na badala yake wana nyundo hao wameamua kumsajili mshambuliaji wa Uruguay na Celta Vigo Maxi Gomez. (Evening Standard)
Leicester imeshinda harakati za kumsaini beki wa klabu ya Luton na Uingereza James Justin kwa dau la £8m ikiwashinda Aston Villa na mabingwa wa ligi ya Uskochi kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mirror)
Mlinda lango wa zamani wa Itali Gianluigi Buffon, 41, yuko katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kurudi katika klabu ya Juventus kutoka PSG ambako alikua katika kandarasi ya mwaka mmoja kama mkurugenzi wa klabu hiyo. (Sky Italia via Football Italia)
Winga wa itali na Roma Stephan El Shaarawy, 26, amekubali kujiunga na klabu ya China ya Shanghai Shenhua kwa dau la £16.11m . (Il Tempo)
Napoli huenda ikaanza kuitumia jezi nambari 10 ya aliyekuwa nyota wa Argentina Diego Maradona wakijaribu kumrai mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez kujiunga na timu hiyo. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa klabu ya Reading na Gambia Mo Barrow ananyatiwa na klabu ya Montpellier na Rennes.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye aliwahi kuichezea ya Swansea City player ya Uingereza pia ananyatiwa na klabu kadhaa za Uturuki na sasa anataka kuondoka katika wafalme hao baada ya miaka miwilii (getreading)
CHANZO.BBC SWAHILI
Social Plugin