Klabu ya Paris St-Germain ipo tayari kumuuza mshambuliaji wake machachari raia wa Brazil, Neymar, 27. (L'Equipe - in French)
Klabu ya Bayern Munich inataka kumsajli kwa mkopo winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale, 29. (Sun)
Kiungo wa klabu ya Lyon Mfaransa Tanguy Ndombele, 22, amesema kuwa anaweza kuhamia Tottenham kama nafasi itatokea. (Telefoot - in French)
Manchester United wanamtaka beki wa kulia wa klabu ya PSV Eindhoven na Uholanzi, Denzel Dumfries, 23. (Sun)
Liverpool wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kufukuzia saini ya kiungo wa klabu ya Besiktas na Uturuki, Dorukhan Tokoz, 23. Tayari ofay a klabu ya Udinese ya Italia ya kutaka kumsaini kiungo huyo imekataliwa na Besitkas. (Fotomac - in Turkish)Philipe Coutinho amekuwa akihusishwa na fununu za kuhama klabu ya Barcelona
Winga huyo wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza kujiunga na Chelsea. (Express)
Kipa mkongwe wa Italia Gianluigi Buffon, 41, amesema anaweza kupumzika msimu mzima kucheza mpira baada ya kukataa ofa ya kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja na klabu ya PSG. (Corriere dello Sport, via Goal)Gigi Buffon ametangaza kuachana na klabu ya PSG
Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi ameonya kuwa hataki tena kuona "tabia za watu mashuhuri" kutoka kwa wachezaji wake. (France Football - in French)
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsajili kipa wa klabu ya Eibar Mhispania Asier Riesgo, 35. (Sun)Asier Riesgo
Kocha wa Inter Milan Antonie Conte anataka kumsajili mlinzi wa zamani wa Chelsea na England Gary Cahill, 33, baada ya beki huyo kuondoka Chelsea.
Cahill na Conte wamewahi kufanya kazi pamoja Chelsea. (Sport Mediaset - in Italian)
Cahill na Conte wamewahi kufanya kazi pamoja Chelsea. (Sport Mediaset - in Italian)
Klabu ya Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa klabu ya Monaco Youri Tielemans.
Tielminas, 22, ambaye ni raia wa Ubelgiji kuanzia mwezi Januari mwaka huu alikuwa kwa mkopo klabu ya Leicester. (Star)Youri Tielemans
Tielminas, 22, ambaye ni raia wa Ubelgiji kuanzia mwezi Januari mwaka huu alikuwa kwa mkopo klabu ya Leicester. (Star)Youri Tielemans
Kiungo wa Everton na timu ya ataifa ya Croatia Nikola Vlasic, 21, anajiandaa kuhamia moja kwa moja klabu ya CSKA Moscow baada ya kuitumikia kwa mkopo kwa msimu mzima. (Championat - in Russian)
Watford wanatarajiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa west Brom Craig Dawson, lakini klabu ya Burnley imetangaza nia pia ya kumsajili beki huyo mwenye miaka 29. (Sun)
CHANZO.BBC SWAHILI
Social Plugin