Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TETESI ZA USAJILI ULAYA JUMATANO



Paris St-German wako tayari kumuuza mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar mwenye umri wa miaka 27 msimu huu. (ESPN)
Real Madrid huenda wakamjumuisha kiungo wa kati Mbrazil Casemiro, 27, kwa ofa yoyote ya kusaini Neymar kutoka PSG. (Marca)

Manchester United watalazimika kulipa hadi pauni milioni 75 wakitaka kumsajili mlinzi Mfaransa Issa Diop,22 kutoka West Ham, baada ya Red Devils kukataa pendekezo la Hammer la kubadilishana wachezaji katika mkataba utakao mhusisha mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23. (Mirror)Martial amefunga mabao 10 katika michuanoyote msimu huu.

Mlinzi wa England na Manchester United Phil Jones, 27, amepelekwa West Ham kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili Diop. (Sun)

Tottenham wamepewa nafasi ya ya kumsajili mlinzi wa Sampdoria Joachim Andersen kwa pauni milioni 31.2 baada ya Arsenal kuachana na mpango wa kusaini kiungo huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 23. (Star)

Everton wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, kutoka Barcelona kwa pauni milioni 22. (Mail)Andre Gomes ameichezea Everton mara 28 msimu huu tangu alipojiunga na Barcelona

Manchester United wanataka Paul Pogba asiondoka katika klabu hiyo lakini akubali kuwa hali inaweza kubadilika waamue kumuuza nyota huyo wa Kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 . (Sky Sports)

Huku hayo yakijiri Real Madrid, wameonywa na rais wao wa zamani, Ramon Calderon kutomsajili Pogba. (Sun)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Leon Goretzka amesema kuwa ''atafurahia sana'' ikiwa klabu hiyo itamsajili winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, msimu huu. (Manchester Evening News)

Ajenti wa Gareth Bale amepuuziliambali madai kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid wa miaka 29 huenda akahamia Bayern Munich kwa mkopo. (Mirror)

Manchester City itampati akadarasi rasmi kiungo wa kati wa Valerenga Oscar Bobb atakaporejea Julai 16. (Mail)

Manchester United wamepatia kipaumbele mpango wa kumsajili mlinzi wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21, kabla ya kuwaangazia wachezaji wengine wanaotaka kuwasajili dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa. (Manchester Evening News)

Roma wanataka euro milioni 70m sawa na paauni (£62.4m) kumnunua Nicolo Zainiolo, 19, amabye amehusishwa na uhamisho kwenda Tottenham. (Calciomercato, via Team Talk)

Meneja wa Rangers Steven Gerrard, 39, amekataa wito wa kocha wa zamani wa Derby County kama kinara wao huku mipango ikifanywa kuziba pengo  litaloachwa na Frank Lampard anaelekea kujiunga Chelsea. (Times - subscription required)

Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumsajili Steve Walsh kama mkurugenzi wa kandanda huku kiungo wa kati wa zamani Darren Fletcher Pia alipewa ofa ya kazi. (Mail)

Southampton wanajiandaa kuipiku Sheffield United na Burnley katika kinyan'ganyiro cha usajili wa mshambuliaji matata raia wa Uingereza Che Adams kwa pauni milioni 14 kutoka Birmingham. (star)

Watford wamewasiliana na PSV Eindhoven katika mpango utakaowezesha kusajiliwa kwa kiungo wa kati wa Uruguay Gaston Pereiro, 24. (Watford Observer)

CHANZO.BBC SWAHILI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com