Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI NA VISIMA SHINYANGA HUSABABISHA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA

NA SALVATORY NTANDU

Katika jitihada za kuhakikisha miundo mbinu ya Maji inalindwa mkoani Shinyanga,jamii imeaswa kutunza vyanzo vya maji na visima ambayo serikali kwa kushiriana na wadau wamevijenga kwa gharama kubwa ili huduma hiyo iweze kuwanufaisha kwa muda mrefu.

Wito huo ulitolewa na Mratibu wa Mipango ya Maendeleo ya Taasisi ya kiislam ya  Istiqaama international Muslimu Community, Wilayani      Kahama  AHMED ALNOOBI wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisni kwake,baada ya Taasisi hiyo kukabidhi visima 200 ambavyo wamekwisha vijenga.

Amefafanua kuwa ,katika kupambana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya majisafi na salama hasa kwa wananchi walioko pembezoni mwa mji(vijijini) wamekuwa wakilkabiliwa na tatizo la maji hali ambayo imesababisha Taasisi hiyo kuchimba visima hivyo 200 ambavyo vimegharimu   shilingi milioni 200.

Amefafanua kuwa Visima hivyo vimejengwa kkatika Halmashauri ya Shinyanga na Kahama mjini lengo likiwa ni kuisaidia jamii ya mkoa wa Shinyanga kuondokana na adha ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama.

Aidha Alnoobi amefafanua kwa Taasisi yake inaendelea kuunga mkono Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais DK JOHN POMBE MAGUFULI ya kumtua mama ndoo ya maji ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya maji safi na salama hususani wale wanaoishio vijijini.

Mbali na hilo amewataka wananchi kuendelea kuitunza miundombinu hiyo ya maji na visima ambavyo vimejengwa,hali ambayo itaendelea kuwatia moyo wadau wa maendeleo na kuendelea kujitoa kwa kujenga visima vingi katika maeneo ambayo yamekuwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama.

Saumu Musa ni Mkazi wa Kahama, amesema kuwa shida ya maji inasabibisha wanawake wwengi kutembea umbali mrefu huku wakiamka  alfajili sana kwenda kutafuta huduma ya maji,jambo ambalo ni  hatari sana kwao kwani wakati mwingine wanakutana wanyama wakali kama vile fisi.

Amesema ndoa nyingi  zilikuwa ziko mashakani kutokana na  dhana ambayo ilikuwa imejengeka hapo awali kwa wanaume kabla ya kujengwa kwa visima hivyo,kuwa wanapokwenda huko asubuhi kutafuta huduma ya mji,kwamba walikuwa wanatuhumiwa na waume zao kuwa wanajihusisha na vitendo vya ngono jambo ambalo sio kweli.

Pius Shija Shil ni mkazi wa kijiji cha Kitwana katika Halmashauri ya mji wa kahama amesema kuwa,kujengwa kwa visima hivyo kumesaidia kuondoa tatizo la kufuata maji umbali mrefu hali ambayo ilikuwa ikisababisha kushindwa kufanya kazi nyingine za uzalishaji mali.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com