SERIKALI SASA KUANZA KUWATAMBUA WAZALISHAJI WADOGO WA UMEME


Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani,akizungumza na watumishi wa Tanesco na wa REA kabla ya kuanza kwa kikao
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,akitoa rai kwa watumishi wa Tanesco na REA katika kikao cha kujadili mambo mbalimbali ya umeme kilichofanyika jijini Dodoma.
katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dk. Hamis Mwinyimvua,akitoa taarifa kwa Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kaleamni kabla ya kufungua kikao cha watumishi wa Tanesco na REA kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kaleamni,akizungumza wakati wa kufungua kikao cha watumishi wa Tanesco na REA kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya baadhi ya watumishi wa Tanesco na REA wakifatilia kwa makini kikao cha Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kaleamni kilichokuwa na lengo la kuwakutanisha na kutatua changamoto mbalimbali za umeme kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
……………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Serikali imesema itaanza kuwatambua wazalishaji wadogo wa umeme na kuwasimamia hata kama wanazalisha umeme kwa kiasi kidogo sana.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodma Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ,wakati wa kikao baina yake na watumishi wa Tanesco na wa mradi wa umeme vijijini REA.

Dkt.Kalemani amesema kuwa ni wajibu wa Tanesco na REA kuwatambua wazalishaji wadogo wa umeme ifike mahali ufanyike utafiti unaoweza kusaidia kuongeza umeme, na wale wenye leseni za EWURA.

“Tuhakikishe kuwa tuwatambue tuwasimamie na tuwaingize, hivyo REA na Tanesco wawasimamie wana mchango mkubwa sana katika hili” amesisitiza Dkt.Kalemani.

Aidha amesema kuwa watendaji hao wameitwa ili kutafakari walichokifanya 2018/2019 na kujipanga upya kutekeleza majukumu yao katika mwaka wa fedha unaoanza Julai ili kuhakikisha huduma zinakuwa imara muda wote.

Dkt.Kalemani amesema kuwa lengo lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunakwenda kutekeleza majukumu yetu ili kutimiza azima ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda bila sekta hii hatuwezi kufikia malengo ya serikali.

Hata hivyo amefafanua baadhi ya changamoto zilizopo katika gridi ya taifa, tumeondokana na mashine kule Ngara bado kuna changamoto watu wanasema bora tubaki na mafuta yetu, tumepeleka gridi kwa lengo la kutatua kero lakini inazidi, Liwale, Geita changamoto zimeonekana.

Aidha amewataka kusimamia suala la kupeleka umeme kwenye taasisi kama vyuo, shule, makanisa, hospitali na taasisi nyingine zikaweze kusaidia jamii ya maeneo husika.

Waziri Kalemani ametaja baadhi ya ajenda moja wapo itakayojadiliwa katika kikao hicho ni utekelezaji wa Sh.27,000 kupeleka umeme vijijini kwa nchi nzima.

“Kuna wateja wa kawaida wanalalamika hawajaunganishiwa umeme miezi miwili au mitatu. mtu katoa pesa yake analalamika tu lazima tukubaliane hapo tukarekebishe na kufikisha umeme katika maeneo yaliyotengwa kwa ajiri ya uwekezaji” amesisitiza.

Pia amesema miradi ya REA inayoendelea kusuasua, ipo inayosuasua, inayokwenda kwa wastani na kwa kasi na wakandarasi wanaoshindwa kufanya kazi tufanye nini, lazima tuchukue hatua kama sereikali.

Amebainisha kuna miradi ya REA awamu ya tatu, mpango wa raundi ya pili uko wapi nani analazimika kufanya nini mpaka sasa kimpango ilitakiwa kuanza julai mwaka huu lazima tujue tunajipanga hilo kwa namna gani.

Aidha Waziri amesema kuwa hakuna mahusiano mazuri kati ya mameneja na wateja lazima mbadilike.

Kwa upande wake katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dk. Hamis Mwinyimvua, amesema kuwa kikao hichi ni kwa ajili ya kupeana maelekezo ya kazi, mahali pa kurekebisha na mahali pa kuongeza bidii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post