Choo cha maturubai cha wachimbaji.
Akina mama wakitafuta mawe ya dhahabu
Na Salvatory Ntandu - Kahama
Zaidi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu 10,000 katika mgodi usiyo rasmi ulipo katika kijiji cha kakola namba tisa katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaindia vichakani.
Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa kijiji hicho Emmanuel
Nkenze wakati akizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea mgodi huo, na kusema kuwa tatizo hilo linahidaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuzuia kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko.
Amesema kuwa vyoo vilivyopo kwa sasa ni madundu kumi ambayo yanaonekana ni machache ukilinganisha na idaidi ya wachimbaji wadogo waliopo ambao wanazidi kuongezeka na kila siku hali huku kasi ya uchimbaji wa vyoo ikiwa ni ndogo huku wengi wao hawatambui umuhimu wa kujisaidia katika maeneo salama.
Baadhi ya wachimbali katika Mgodi huo akiwemo Samwel
Joseph na Esta Shija wamesema kwa sasa hali sio nzuri katika eneo hilo kwani wachimbaji wengi hawana desturi ya kujisaidia katika vyoo na kuziomba mamlaka husika kulipatia ufumbuzi wa haraka ili kuzuia watu kupata magonjwa kwani idadi ya wachimbaji inazidi kuongezeka.
Wamefafanua kuwa gharama za kujisaidia katika vyoo vilivyopo katika eneo hilo ni kubwa jambo ambalo wao wameshindwa kuimudi kwani zinabadilika badilika mara kwa mara katika vyoo vilivyopo katika maeneo hayo na kusababisha wengi wao kwenda kujisaidia vichakani.
Naye Msimamizi mkuu wa Mgodi huo Husein
Makubi Ngh’wananyazala amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa kwa sasa ofisi yake imewekeza nguvu kubwa katika ujenzi wa vyoo ili kukabiliana na Tatizo la uhaba wa matundu ya vyoo ikilinganishwa na idadi kubwa ta wachimbaji.
Hata hivyo amesema kuwa, tatizo la upungufu wa vyoo mgodini umetokana na uongezeko la wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakiongezeka kila siku kutokana na eneo hilo kuwa na wingi wa madini.
Amesema kuwa, ili kuendelea kupamaba na uhaba huo wameanza kuwahamasisha wamilikiwa wa nyumba za kulala wageni zilizojengwa katika eneo hilo,kuhakikisha wanajenga vyoo kabla ya kufungua nyumba yake ali ambayo itapunguza adha ya wachimbaji kujisaidia vichakani.
Akiongea kwa niaba ya wachimbaji wadogo Samweli Joseph alisema kuwa, sababu inayopolekea wachimbaji wadogo kujisadia vichakani,inatokana na gharama ya shilingi 3,00 za kujisaidia katika vyoo viliyopo na kufanya wengi wetu kujisaidia vichakani
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi
Macha amesema kuwa ujenzi wa vyoo katika Mgodi huo unandelea kujengwa kwa haraka ili kuhakikisha Tatizo hilo linakomeshwa mara mmoja.
Social Plugin