Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wameushambulia uwanja wa ndege wa Abha ulioko kusini magharibi mwa Saudi Arabia, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine saba.
Taarifa hizo ni kulingana na SPA, shirika la habari la serikali la Saudi Arabia.
Awali waasi hao wa Houthi walisema kwamba wamefanya mashambilizi ya ndege zisizotumia rubani katika viwanja vya ndege vya Abha na Jizan, vyote viwili vikiwa karibu na mpaka wa Yemen.
Hata hivyo, Saudi Arabia haikutaja taarifa zozote za mashambulizi katika uwanja wa ndege wa Jizan. Muungano wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia umelieleza shambulio hilo kuwa ni la kigaidi.
Mapema mwezi huu, waasi wa Houthi walifanya mashambulizi ya makombora katika uwanja wa ndege huo wa Abha, na kujeruhi watu 26.
Social Plugin