Na Amiri kilagalila-Njombe
Shirika la kuhudumia viwanda vidogo mkoani Njombe SIDO limesema lipo hatarini kupoteza zaidi ya mil 100 ambazo zilikopeshwa kwa wajasiriamali, wabunifu na wamiliki wa viwanda vidogo ili kuongeza mitaji ya biashara zao kwa kuwa limebaini idadi kubwa ya wakopaji walikuwa wakitoa taarifa za uongo na kugushi nyaraka.
Akizungumzia changamoto hiyo meneja wa SIDO mkoani humo Isdori Kiyenze amesema mwaka uliopita shirika hilo lenye dhamana ya kuwainua kimitaji wajasiriamali na wamiliki wadogo wa viwanda lilitoa mikopo yenye thamani ya mil 250 ambapo katika kiwango hicho mil mia moja na laki nane hazijareshewa hadi sasa huku akidai katika uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kuwa wengi wao hawakuwa waaminifu kwa kuwa wamegushi nyaraka pamoja na dhamana zao,huku wengine wakishindwa kurejesha mikopo yao kwa kutumia pesa nje ya malengo ya mkopo.
Kutokana na hali hiyo inayokwamisha mpango wa serikali wa kuwainua kiuchumi na mitaji ya wajasiriamali na wamiliki wadogo wa viwanda nchini meneja huyo anataJa hatua ambazo shirika kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zimeanza kuchukuliwa dhidi ya wadaiwa sugu na kueleza jinsi hali hiyo inavyowakosesha haki ya kukopeshwa wahitaji wengine waaminifu.
"Tunaenda hatua kwa hatua,na itafikia mpaka kuuza zile dhamana zao na sasa yamekwishabandikwa matangazo, haya mfano hata huduma zingine usipo lipa maji unakatiwa na usipolipia umeme unakatiwa na usipolipa mkopo tutachukua dhamana zako ili hela ya serikali iludi na kuendelea kuwakopesha wengine"amesema Isdory kiyenze
Baadhi ya wajasiriamali akiwemo Joyce Chumi na Selini John wanasema vikwazo vinavyo likumba shirika la SIDO katika ukusaji wa fedh hiyo imesababishwa na uwepo wa mfumo mbovu wa utoaji wa mikopo hiyo huku wakidai kwamba imekuwa ikitolewa kisiasa zaidi.
"Watu waliopewa mikopo ya Sido walichukuliwa bila utaratibu mzuri,wengi waliopata hawakustahili,sasa unampa hela mtu asiyekuwa na mtaji unategemea nini?utakuta anachukua pesa anaenda kununua vitenge"amesema Joyce Chumi
Tayari mpango wa kuanza kuuza dhamana za wadaiwa sugu unategemewa kuanza ili kunusuru upotevu wa fedha hiyo ya serikali
Social Plugin