Mkurugenzi wa shule ya Southern Highlands Mafinga Mary Mungai (wa tano kulia) akiwa na wazazi wa na marafiki wa wanafunzi Mariam Wambura na Stephen Sanga ambao waliwakilisha shule za Tanzania katika kongamano la dunia la mazingira nchini Finland wa kwanza kulia ni mkuu wa msafara wa wanafunzi hao Kitova Mungai .
Wanafunzi wa shule ya Southern Highlands Mafinga na viongozi wao wakiwa katika eneo lilolohifadhiwa katika misitu ya Sao Hill Mufindi wakijifunza jinsi ya utunzaji wa mazingira.
wanafunzi wa shule ya Southern Highlands Mafinga na viongozi wao wakiwa katika eneo lilolohifadhiwa katika misitu ya sao Hill Mufindi wakijifunza jinsi ya utunzaji wa mazingira
***
Na Francis Godwin,Iringa
Uongozi wa shule ya Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa umesema unakamilisha utaratibu wa kukabidhi azimio la dunia lililokabidhiwa kwa wanafunzi wawili wa darasa la saba katika shule hiyo Mariam Wambura na Stephen Sanga ambao waliliwakilisha shule za Tanzania nchini Finland katika Tanzania kongamano mazingira kwa la shule za msingi duniani.
Mkuu wa msafara wa wanafunzi hao nchini Finland ,Kitova Mungai ambaye ni mmoja wa mkurugenzi wa shule hiyo alisema kuwa wanafunzi hao Mariam Wambura na Stephen Sanga wamerejea nchini baada ya kushiliki katika kongamano hilo la siku 10 nchini Finland.
Alisema kongamano hilo la siku kumi la wanafunzi kuhusu utunzaji mazingira limehitimishwa kwa kutoa azimio kwa wanafunzi kuhusu utunzaji wa mazingira azimio hilo ambalo litawezesha dunia kuwa katika hali nzuri ya ustawi wa mazingira duniani.
Alieleza kuwa azimio hilo limelenga kuhamasisha shule na jamii kuendelea kutunza mazingira ili kuwezesha kizazi cha baadae kuishi katika mazingira salama yasiyo na uharibifu wa mazingira.
"Tumekuwa tukiwafundisha masomo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira na wamekuwa wakiotesha miche ya miti na kuisambaza maeneo mbali mbali ya shule ",alisema Mungai.
Kutokana na kazi hiyo ya utunzaji mazingira ndio iliyowezesha shule hiyo wanafunzi wake kuteuliwa na waandaaji wa kongamano hilo kwenda nchini Finland kushiriki kongamano hilo la dunia kwa niaba ya shule zote Tanzania.
Hata hivyo alisema wanakusudia azimio hilo ambalo walipewa na waandaaji wa kongamano hilo kuliwasilisha serikalini ili kulisambaza kwenye shule zote nchini kwa kupitia viongozi wa serikali ya Tanzania ili shule zote kuweza kutekeleza maagizo yaliyitolewa kwenye kongamano hilo la dunia.
Mungai alisema azimio hilo limegawanyika katika sehemu kuu tatu ikiwemo ya kuangalia uwezekano wa kuondoa kaboni katika hewa ili kuona jinsi ya kuidaka hewani na kuihifadhi sehemu ili isilete madhara mbeleni , sehemu ya pili ya azimio ni kupunguza kaboni hiyo katika mazingira yetu na sehemu ya tatu ni kuweka utaratibu mzuri wa kuwasiliana kati ya wanafunzi wa Tanzania na wale wa nchi nyingine .
" Azimio hili tunategemea kulikabidhi kwa mawaziri wa serikali ya Rais Dkt John Magufuli akiwemo waziri wa elimu ,waziri wa TAMISEMI na waziri wa mazingira ili kuweza kulisambaza azimio hili kwa shule zote za msingi nchini na kwenye Halmashauri na mikoa ili kuanza utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira", alisema.
Wakiwa katika kongamano hilo la wanafunzi duniani walipata nafasi ya kushiriki kongamano jingine la kuangalia viwanda duniani vinafanyaje katika maeneo yao kuhakikisha wanazalisha bila kuharibu mazingira kongamano ambalo baloz wa Tanzania anayewakilisha nchi kama tano ikiwemo ya Sweden nchini Dr. Wilbrod Peter Slaa alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo kubwa .
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Mary Mungai alisema kutokana na heshima kubwa ambayo shule yake imeipata ya kuwakilisha Taifa katika kongamano hilo la dunia watahakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira na kuwa azimio hilo wataanza kulifanyia kazi wao ili wengine wafike kujifunza .
Wanafunzi walioshiliki katika kongamano hilo Mariam na Stephen walisema tofauti ya nchini ya Finland na Tanzania katika uhifadhi wa mazingira ni kubwa kwani wakiwa katika kongamano hilo waliweza kujifunza na kuzunguka mitaa mbali mbali kuona jinsi wananchi wa Finland wanavyozingatia uhifadhi wa mazingira kwa kutenga vyombo vya kuhifadhi taka ngumu ,taka laini na taka nyingine na sio kama ilivyo Tanzania kwa maeneo mengi kuwa na chombo kimoja cha taka kinachotupwa taka zote .
Pia walisema kwa upande wa vyombo vya moto mfano magari kuwa nchini Finland magari yao yanatumia umeme na sio mafuta kama ilivyo Tanzania na kuwa wanatumia magari hayo yanayotumia umeme kama njia ya kulinda usafi wa mazingira yao.
Social Plugin