Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa tiba ya bure kutoka kwa madaktari na wauguzi kutoka nchi Mbalimbali walioweka kambi ya uchunguzi katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa uzinduzi huo |
Katibu wa Afya Mkoa wa Tanga Abdy Makange akizungumza wakati wa uzinduzi huo |
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Anisa Mbega kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu |
Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy akizungumza wakati uzinduzi huo |
WANANCHI wametakiwa kujenga utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini aina ya magonjwa wanayokabiliana nayo ili kuweza kuanza tiba mapema kabla ya ugonjwa kukithiri.
Hayo yamebainishwa na wakati wa uzinduzi wa tiba ya bure kutoka kwa madaktari na wauguzi kutoka nchi Mbalimbali walioweka kambi ya uchunguzi katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza.
Jopo hilo la wahudumu wa afya ambalo linaratibiwa na taasisi ya Head INC yenye maskani yake nchini Marekani lipo wilayani humo kwa ajili ya kuchunguza afya za wakazi wa wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mratibu wa Head Inc (Diaspora) Asha Nyanganji alisema kwamba lengo la ziara hiyo kutoa elimu na huduma za afya wataalamu waliokuwa wanafanyakazi na wataalamu wa hapa kwetu na hivyo kubadilisha uzoefu.
Aidha aliwataka watanzania kuweka utaratibu wa kuangalia afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini magonjwa yanayowasumbua ili kuweza kupata matibabu mapema badala ya kusubiri mpaka wanapozidiwa.
Awali akizungumza kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Anisa Mbega lengo la madhumuni ya ziara hiyo utakumbuka serikali imekuwa ikijitahidi sana kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali ikiwemo za afya.
Alisema wao kama Wizara ya nje kupitia Diaspora kubwa ni kuhamasisha Diaspora popte waliop nje ya nchi kurudi nyumbani kurudisha walichokichuma ikiwemo ujuzi na kutoa ujuzi na utaalamu wao kupitia hiyo walikuwa wakiwashirikisha madaktari ambao wamekuja na kufanya ziara zao ambazo zinalenga kutoa huduma za afya na kutoa ushauri.
Magonjwa ambayo walikuwa wakitazama ni pamoja na saratani ya uzazi na matiti,ugonjwa wa meno na huduma mbalimbali na wameona kuna shida na uhitaji mkubwa wa wananchi kupata matibabu hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo amesema kuwa serikali imekuwa ikifanya maboresho makubwa katika sekta ya afya lengo ni kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora .
Nae Mbunge wa jimbo hilo Balozi Adadi Rajabu aliwataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka ili waweze kujua hali zao.
Kambi ya matibabu ya bure inatarajiwa kuwepo kuanzia Juni 21 hadi 25 natayatri jumla ya wananchi 450 wamejitokeza kupatiwa matibabu hayo huku magonjwa ya macho na kinywa ndio yameoneka na waathirika wengi.
Social Plugin