Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuchangamkia fursa ya kutengeneza mifuko mbadala kwa kuwa mahitaji ni makubwa na soko ni kubwa.
Majaliwa amesema hayo jana Ijumaa Juni 28, 2019 wakati akitoa hoja ya kuahirisha kikao cha mkutano wa 15 wa Bunge la Tanzania.
Amesema uzalishaji wa mifuko hiyo hautoshelezi mahitaji kwa sasa.
Majaliwa amesema utekelezaji wa katazo la Serikali ya Tanzania la mifuko ya plastiki limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, wananchi wameonyesha mwitiko wa hali ya juu kutumia mifuko hiyo.
Amesema jumla ya viwanda 11 vimejikita kwenye uzalishaji wa mifuko mbadala 10 vikiwa Dar es Salaam na kimoja Arusha.