Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mpaka kufikia mwezi januari 2019 hadi machi 2019 jumla ya makosa 113 dawa za kulevya yaliripotiwa hapa nchini na watuhumiwa 1,842 wa makosa ya dawa za mirungi na bangi.
Hayo yamesemwa leo Juni 17,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa viti Maalum ,Zainabu Katimba aliyehoji serikali ya awamu ya tano tangu iingie Madarakani imebaini na kuwachunguza watu wangapi wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kuleya.
Katika majibu yake Yake,Mhandisi Masauni amesema tokea serikali ya awamu ya tano iingie Madarakani imewabaini makosa 679 na kuwakamata watuhumiwa 1,269 kwa mwaka 2016,Makosa 902, na watuhumiwa 1,578 mwaka 2017,Makosa 702 na watuhumiwa 886 kwa mwaka 2018 ,makosa 113 na watuhumiwa 1,842 kwa mwaka 2019.
Aidha,Mhandisi Masauni amesema madawa mashambani Mirungi na bangi yaliyokamatwa kwa mwaka 2016 ni jumla ya makosa 10,375 na watuhumiwa 26,031,makosa 8,956 na watuhumiwa 12,529 kwa mwaka 2017,makosa 7,539 na watuhumiwa 9,987 kwa mwaka 2018.
Baadhi ya watuhumiwa wamepelekwa mahakamani na wengine upelelezi wa Mashauri yao unaendelea huku Jeshi la polisi kupitia Programu ya kuzuia uhalifu limeendelea kutoa huduma ya urekebishaji kwa waathirika wa dawa za kulevya.
Kwa upande wake Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu ,vijana,ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amesema ofisi ya Waziri mkuu imefanikiwa kudhibiti dawa za kulevya kwa asilimia 95% huku waathirika wote wa dawa za kulevya wakipewa elimu pamoja na kufanya kazi ili kurejea katika hali yao ya kawaida.
Social Plugin