Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZAZI WAPIGWA MARUFUKU KUFANYA BIASHARA NA WATOTO WADOGO SOKONI


Uongozi wa soko kuu la mitumba la Memorial, Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, umeahidi kushirikiana na jeshi la Polisi kupiga marufuku wafanyabiashara wa soko hilo kwenda sokoni hapo na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa soko hilo, Godfrey Shayo, leo Juni 24, wakati wa utafiti wa kuongeza uelewa, uwajibikaji wa huduma bora za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto (ECD),  zoezi linalo tekelezwa na muungano wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) kwa kushirikiana na taasisi ya CIC ya Ireland

“Ukija sokoni hapa majira ya saa 11 Alfajiri utaona wazazi na walezi wakiwa na watoto wachanga huu ni ukatili na unaathiri afya ya mtoto na malezi yake ya baadaye, tumeliona hili na tunaandaa mpango wa kutoa elimu kabla ya kuchukua hatua” amesema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa masoko la Mbuyuni, Lameck Mziray na mwenyekiti mtaa wa soko la Pasua, Rahibu Juma walikiri kuwapo kwa changamoto inayoathiri afya za watoto hao lakini wameahidi kuandaa mpango wa ushirikishwaji na wafanyabiashara ili kujadili suala hilo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com