Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli jijini Dar es salaam kutumia fursa ya kibiashara itakayotokana na ujio wa wageni zaidi ya 1,000 watakaoshiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Agosti 2019.
Profesa Kabudi ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli.
Amesema wizara yake itafanya kazi kwa ukaribu na wadau hao na kuwataka kutoa huduma bora.
Waziri huyo amewataka wamiliki na wafanyabiashara hao wa hoteli kuzingatia mwongozo wa Serikali uliotolewa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusiana na suala la ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa kuwataka kuwaelekeza wageni kubadilishia fedha zao benki na pia katika hoteli ambazo zimeidhinishwa kubadilisha fedha za kigeni.
Social Plugin