Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ameachia uongozi wa chama tawala cha Conservative hii leo hatua inayofungua mlango wa kinyang'anyiro cha mrithi wa nafasi hiyo.
May hatauhutubia umma lakini amewasilisha barua ya kuthibitisha kujiuzulu kwake kwa kamati ya chama chake yenye nguvu ijulikanayo kama "Kamati ya 1922".
May ataendelea kuwa waziri mkuu hadi wabunge watakapomchagua kiongozi mpya wa chama hicho mchakato utakaouchukua hadi miezi miwili.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson anapewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hiyo.
Waziri Mkuu May alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo Mei 24 baada ya kushindwa kufanikisha makubaliano ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya ama Brexit.
Social Plugin