Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA SC YANASA KIFAA KUTOKA ALLIANCE FC

Klabu ya Yanga imeendela kujiweka sawa kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania Bara pamoja na michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika kwa kunasa saini ya baadhi ya wachezaji na safari hii wakinasa saini ya mchezaji mwingine mzawa. 

Kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani,imemtambulisha Balama Mapinduzi kuwa mchezaji wake mpya ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu kukipiga na klabu hiyo. 


Balama Mapinduzi msimu uliopita alikuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao waliing’arisha Alliance Fc ya jijini Mwanza,na kuifanya imalize ligi kuu soka Tanzania Bara katika nafasi nzuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com