Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema baada ya kufuatilia sakata la mauaji ya Watanzania waliokuwa wakiishi Msumbuji amesema tayari, watu Watano (5) wamekamatwa huku mmoja akiuawa kufuatia msako mkali kati ya Polisi wa Tanzania na Msumbiji.
Ameeleza hayo leo wakati Rais Magufuli anazindua rasmi nyumba 15 za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo Mkoani Geita.
“Kumekuwa na upungufu mkubwa sana wa matukio ya uhalifu kwa mwaka jana ikilinganishwa na mwaka huu, ninakushukru Mh.Rais kwa kukubali mualiko wangu wa kuja kutuzindulia hizi nyumba 20 ambazo kwetu ni za muhimu sana na ninaamini zitaongeza morali wa watendaji wetu.
"Lile tukio lililonipeleka Msumbiji, niliahidi kwa Watanzania kwamba damu ya Mtanzania haipotei, nikuhakikishie Mhe. Rais hadi sasa watano wameshakamatwa na mmoja ameshatangulia mbele za haki, na wanatajana, plan yote ilifanyika hapa kwetu" alisema IGP Sirro.