Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Tafiti zinaonesha asilimia 74.4 hawana uelewa wa kutosha kuhusu fedha za maendeleo ya vijana nchini.
Kati ya vijana 6,265 waliohojiwa wakati wa utafiti ni vijana 4,659 sawa na 74.4 hawana uelewa wa kutosha kuhusu fedha za maendeleo ya vijana yanaonesha kuwa kuna kiwango kidogo cha uelewa.
Mratibu msaidizi wa mradi wa Restless Development Denice Simeo ameyasema hayo Jana Julai 26,2019 alipokua akizungumza na wandishi wa habari kwenye ukumbi Lawate jijini Dodoma.
Aidha Denice Simeo ametoa mapendekezo kupitia matokeo ya utafiti huu, ambapo amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana ,wawekeze katika utoaji wa elimu.
Pia Vijana wametakiwa kujenga utamaduni wa kuhakiki vyanzo vya taarifa kabla ya kuzifanyia kazi hasa zile zinazowekwa katika mitandao ya kijamii ambapo Simeo amesema kupitia matokeo ya utafiti uliosimamiwa na kuongozwa na vijana umebaini kuwa mara nyingi vijana hupokea taarifa bila kufanya uhakiki wa taarifa hizo.
Hivyo utafiti huo ulitoa mapendekezo kwa vijana kuwa ,taarifa ambazo zinatolewa wanatakiwa kutengeneza mazingira ya kuhakikisha na kujiridhisha kuwa yana uhakika kiasi gani ili kuweza kuchukua maamuzi yaliyo sahihi.
Hata hivyo Bw.Simeo amesema kuwa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kama mashirika binafsi wanapaswa kusaidia kuboresha mfumo wa utoaji wa upatikanaji wa taarifa kuhusu fedha za miradi ya maendeleo ya vijana kwa makundi yote ya vijana ili kuwezesha uwepo wa taarifa za kutosha kwa walengwa.
Taasisi ya Restless Development ilifanya utafiti juu ya jitihada za serikali katika kumuwezesha kijana kiuchumi, kwa kuangalia fedha za maendeleo ya vijana zinazotengwa iwapo zinawafikia walengwa.
Utafiti huo ulilenga kutathmini jitihada za uwezeshaji wa vijana kiuchumi kupitia fesha za maendeleo na kuhusisha halmashauri nne ikiwemo Manispaa ya kinondoni ,Kigamboni ,Morogoro huku ikiwafikia vijana zaidi ya elfu sita.
Katika hatua nyingine,baadhi ya vijana wamesema kuwa ,mwitikio mdogo wa kuomba mikopo unasababishwa na sababu mbalimbali zikiwemo woga wa kufanya biashara pamoja na elimu hafifu kwa vijana hao hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana.
Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya waziri mkuu, kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu na halmashauri zote nchini inafanya jitihada kubwa ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kutenga fedha n akuweka mazingira rafiki kwa vijana ili kunufaika na fedha hizo na kujikwamua kiuchumi.