SALVATORY NTANDU
Kushuka kwa bei ya Pamba nyuzi katika Soko la dunia kumetajwa kuwa ndio chanzo cha makampuni ya ununuzi wa zao la Pamba mkoani Shinyanga kushindwa kununua kwa kuogopa kupata hasara.
Hayo yamebainishwa na Amiri Mwinyimkuu Meneja Shughuli wa Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kahama kuhusiana na hatua walizichukua ili kukabiliana na tatizo hilo.
Amesema kwa sasa Kampuni za ununuzi wa zao hilo zimeshindwa kwenda sokoni kununua pamba kutokana na kushuka bei ya Pamba nyuzi katika soko la dunia hali ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kufunguliwa kwa soko la Pamba.
Amefafanua kuwa bei ya pamba nyuzi katika soko la dunia kwa sasa ni dola 1.39 ambayo ikibadilishwa kwa fedha za kitanzania ni shilingi 1,449 hivyo endapo watanunua pamba mbegu kwa shilingi 1,200 watapa hasara.
Ameongeza kuwa kampuni hizo zimeomba bei ya kununua kwa mkulima ishuke sokoni au serikali iwape kinga (guarantee) ya kuwafidia hasara itakayopatika baada ya kuuza pamba katika soko la dunia ambapo hadi sasa bado serikali haijatoa maekekezo yeyote.
Katika hatua nyingine Mwinyimkuu amesema wakulima katika wilaya ya kahama wamelima pamba ekari 40,869 na wanatarajia kuvuna kilo zaidi ya milioni 400.
Makampuni yaliyopatiwa leseni za kununua pamba hizo ni Kahama Cotton Campuny Limited (KCCL) Kahama Oil Mill, Afriacian na kampuni ya Fresho ambapo mpaka sasa kampuni mbili ndio zimeweza kununua zao hilo ambazo ni Fresho na Kahama Oil Mills.
Social Plugin