Bondia wa Russia, Maxim Dadashev amefariki baada ya kupata majeraha makubwa.
Dadashev aliyekuwa na umri wa miaka 28, alifariki baada ya kupata kipigo alipokuwa akizichapa na mpinzani Subriel Matias London, England.
Dadashev aliondolewa kwa msaada wa machela akionekana mwenye hali mbaya.
Bondia huyo alivuja damu ndani ya ubongo na licha ya kufanyiwa upasuaji haraka, alifariki dunia.
Taarifa ya Russia ilisema inafanya uchunguzi wa tukio la bondia huyo kama kulikuwa na viashiria vya vurugu vilivyotokea ulingoni.
“Tumesikika kumpoteza bondia mwenye umri mdogo aliyekuwa hodari ulingoni, tunaungana na familia ya Maxim Dadashev,”alisema Katibu Mkuu Umar Kremlev.
Bondia huyo amefariki akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yote 13 aliyocheza enzi ya uhai wake.
Social Plugin