Breaking : RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA JANUARY MAKAMBA.....BASHE ATEULIWA KUWA NAIBU WAZIRI WA KILIMO

 Rais wa  Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dkt. John  Pombe Magufuli leo Jumapili Julai 21, 2019 amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri kwa kuwateua mawaziri wapya mawili.

Taarifa ya mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ameteuliwa kuwa naibu Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda.

Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuchukua nafasi ya January Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia, Rais Magufuli amemteua Balozi Martin Lumbanga kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA).

Balozi Lumbanga ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili. Taarifa hiyo inaeleza kuwa uteuzi huo umeanza leo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post