Na Amiri kilagalila-Njombe
Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kimesema mapema wiki ijayo kinategemea kufika mahakamani kupinga utaratibu uliyotumika kumvua ubunge aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Antipas Lissu ambaye yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu baada kushambuliwa na watu wasiojulikana mwaka jana katika eneo la eria D jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa chama hicho John Mrema wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mkoani Njombe akiwa ameambatana viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa chama hicho freeman mbowe ambaye amefanya mkutano wa ndani mjini humo.
Mrema amesema kuwa chama hicho kinaona kuwa utaratibu huo umekiuka sheria kwa sehemu kubwa kwakuwa utenguzi huo umefanyika wakati mbunge huyo akiwa katika matibabu na kwamba kuhusu kujaza fomu za maadili na mali amesema asingeweza kujaza kwa kuwa hakuwa ndani ya nchi na asingeweza kusainiwa kwa mujibu wa sheria
Amesema Agenda nyingine ambazo zinajadiliwa katika ziara hiyo katika kanda ya Nyasa ni pamoja uchaguzi wa serikali za mitaa,kuwashukuru viongozi na wanachama kwa kazi kubwa waliyofanya wakati mbowe na viongozi wa chadema wakiwa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne pamoja na kutoa ufafanuzi wa sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo imeonyesha kubadili kwa kiasi kikubwa utendaji wa vyama nchini.
Nao baadhi ya viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo Rose Mayemba kiongozi wa chadema msingi na Alatanga Nyagawa ambaye ni katibu wa mkoa chama wamesema wameanza kuandikisha wanachama katika daftari la maalumu la A3 kuanzia ngazi ya chini na kwamba watanzania wategemee chama hicho kupata ushindi mkubwa kwa kuwa kimejihimarisha katika utunzaji wa taarifa.
Katika ziara hiyo Mbowe amekagua ujenzi wa jengo la ofisi za chama iliypo katika mtaa wa hagafilo ilyofikia asilimia 95 katika ujenzi wake
Social Plugin