Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Edward Mpogolo aliyeteuliwa jana usiku na Rais Magufuli ameapishwa leo Julai 25,2019 zoezi lililofanyika katika makao Makuu ya nchi,Dodoma.
Akizungumza wakati akimwapisha mkuu huyo mpya wa Wilaya ya Ikungi ,Mkuu wa Mkoa Wa SINGIDA Rehema Nchimbi amesema amesema amempongeza Mkuu Mpya wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa katibu tawala wilaya ya Dodoma Mjini.
Hivyo, Mhe.Nchimbi amemtaka mkuu huyo mpya wa wilaya kutekeleza majukumu yake katika miradi mbalimbali ya wilaya ya Ikungi ili kuwaletea Maendeleo ya Wananchi.
“Singida ni makao makuu mwenza ya Tanzania ,sasa wewe mkuu wa wilaya Edward Mpogolo ni kuwahakikishia watanzania kuwa Singida sio kame,Singida sio masikini,Singida sio njaa.Singida imekuwa ikipokea fedha nyingi kama mikoa mingine kwani kwa ndani ya miaka minne imepokea zaidi ya Tsh.bilioni mia saba kwa ajili ya Maendeleo “alisema Nchimbi.
Aidha ,Mkuu huyo wa Mkoa Wa Singida amemtaka mkuu mpya wa Wilaya ya Ikungi kwenda kusimamia mkakati kabambe wa Mkoa Wa Singida ambao umeanzishwa kwa lengo la kupunguza kero za mishahara kwa watumishi ujulikanao kama”Mshahara wangu Uko wapi “huku pia akimtaka kwenda kutatua na kusimamia suala la kilimo hususan kilimo cha Alizeti na korosho Pamoja na Sekta ya kilimo.
Kwa upande wake Mkuu mpya wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo ameahidi kuwa ataenda kushirikiana na halmashauri ya Ikungi katika kusimamia miradi mbalimbali na kuongeza makusanyo ya halmashauri ili kwa ajili ya Maendeleo ya nchi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mpogolo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, nafasi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma itajazwa baadaye.
Ikumbukwe kuwa hapo jana Julai 24,2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Bw. Edward Mpogolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida ambapo Mpogolo anachukua nafasi ya Bw. Miraji Mtaturu ambaye amechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki lililokuwa linaongozwa na Tundu Lisu [CHADEMA ]ambapo umbunge wake ulifutwa.
Social Plugin