Mti maarufu uliopo katikati ya kijiji cha Gambosi 'Gamboshi' ,kata ya Gambosi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu ambao unadaiwa kuwa watu huwa wanapotea katika mazingira ya kutatanisha wakipita karibu na mti huo.
Waganga wa jadi kutoka Gamboshi na wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wametoa onyo kali kuwa watampoteza mwanachama yeyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), atakayethubutu kuchukua fomu ya kugombea urais mwaka 2020 na kumpinga Rais John Magufuli.
Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi mkoani Simiyu,Bwimila Shala amesema:
"Sisi ni waganga wa jadi wilaya ya Bariadi ,ni Wazee wa jadi ambao wanaungana na Mheshimiwa Rais,kuhakikisha kwamba dua hii tunayoizungumza leo au kumuombea...tunahakikisha mwaka huu na mwaka unaokuja kwenye uchaguzi tunamlinda na yeyote yule atakayechukua fomu bila utaratibu wa waganga wa tiba asili tutampoteza kwa njia yoyote ile".
TAZAMA HAPA ZAIDI
Kuhusu Gamboshi/Gambosi
Inasemekana Makao makuu ya uchawi Tanzania ni Kijiji cha Gamboshi. Kijiji hiki kinavuma kwa uchawi kanda ya ziwa na Tanzania. Kijiji hiki kuna imani kwamba usiku hung'aa na kuonekana kama Jiji la New York wakati hakuna hata nguzo moja ya Umeme.
Watu wa kijiji hiki huamini uchawi ndo kila kitu kwao,
huwezi kuingia kijiji hiki bila kuonana na wenyeji kwanza,
na inaelezwa kuwa ukifika wilaya ya Bariadi ukauliza nataka kwenda kijiji cha Gambushi lazima watakuuliza hili swali " Unakijua lakini kijiji hicho".