Mnano tarehe 14/07/2019 majira ya saa 09:00 huko Kanyegele kata ya kiwira tarafa ya Ukukwe wilaya ya Rungwe. Barabara ya kuu ya TUKUYU – MBEYA, Gari na. T. 359 DCA/T. 429 CMH Aina ya Howo mali ya kampuni ya “Overland” iliyopo “Dsm” ikiendeshwa na RAJAB S/O ISSA [40] ikiwa imebeba mafuta aina ya Petrol na Diesel kuelekea Tukuyu iliacha njia na kupindukia kolongoni na kusababisha uharibifu wa mali na mafuta kumwagika baada ya “Tank” kupasuka. Aidha msaidizi wa dereva aitwaye SALUMU S/O SAID[40] amepata majeraha. Chanzo cha ajali ni ubovu wa matairi ya gari hiyo.
Natoa wito kwa wananchi kutosogea maeneo ya ajali bila kuchukua tahadhari, kwani madhara ya kufanya hivyo ni kupata ulemavu wa viungo, au kupoteza maisha kutokana na hatari mbalimbali kama milipuko ya mafuta.
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO- WILAYA YA MBALIZI.
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 20:30 u0siku, CHRISTINA D/O ANTHONY @ MWALINGO [37] aligongwa na gari huko katika Kata Inyala, Tarafa Tembela, Wilaya Kipolisi Mbalizi, Mkoa Mbeya, barabara ya Mbeya – Njombe na kusababisha kifo chake papohapo. Gari na dereva hajafahamika. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Igawilo. Ufuatiliaji kumkamata dereva na gari unaendelea.
TUKIO LA MAUAJI -WILAYA YA MBEYA.
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 09:00 asubuhi huko meneo ya mtaa wa Mponja Kata ya Igawilo, Tarafa Iyunga, Jijini Mbeya, mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la MARIA D/O FAUSTINE@KISANJI [22] Mkazi wa Mwanyanje alikutwa amefariki dunia kwenye Pagala linalomilikiwa na mtu aitwaye ESTER D/O JOHN @MWANSHEMELA
Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa mhudumu wa Bar itwayo SIKALAMANGA inayomilikiwa na DOMINICK S/O ABRAHAM.Ambapo mnamo tarehe 13/07/2019 majira ya saa 23:00 usiku marehemu aliondoka na mtu asiyefahamika/jinsia ya kiume ambaye alikuwa anakunywa naye pombe. Kiini cha tukio ni ugomvi wa kimapenzi kati ya wawili hao. Msako mkali unaendelea ili kubaini na kumkamata aliyehusika katika tukio hilo.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na wahalifu kwa kuweka mkazo zaidi katika kutoa elimu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani.
WITO:
Natoa wito kwa jamii kuacha, kujihusisha na vitendo vya kihalifu na kujishughulisha na kazi halali kwa ajili ya kujipatia kipato. Ni rai yangu kwa wananchi/Madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuchukua tahadhari pindi wanapokuwa katika barabara zenye miteremko mikali, na milimani kwani ajali nyingi hutokea maeneo hayo na kusababisha madhara makubwa kwa jamii.
Imesainiwa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Social Plugin