Serikali imesema homa ya dengue imeua watu 13 nchini huku 6,677 wakiugua ugonjwa huo.
Takwimu hizo zimetolewa jana Jumamosi Julai 27, 2019 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa kupambana na mbu na wadudu wengineo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Waziri Ummy alisema awali takwimu zilionyesha vifo sita lakini Serikali ilifanya tathmini upya na kupata takwimu sahihi..
Alisema ugonjwa huo kwa sasa unapungua kwa maelezo kuwa Juni, 2019 kulikuwa na wagonjwa 536 na tangu kuanzia Julai hadi leo kuna wagonjwa sita pekee.
Social Plugin