Chama cha Mapinduzi, CCM kimemteua Miraji Mtaturu kuwa mgombea ubunge wa Singida Mashariki.
Taarifa iliyotolewa na katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema kikao cha Kamati Kuu kimekutana leo Jumanne Julai 16, 2019 chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli jijini Dodoma kikiwa na agenda moja.
Polepole amesema agenda hiyo ilikuwa ni ya maandalizi ya uchaguzi huo kwa kuteua jina la mgombea ambapo Mtaturu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Ikungi mkoani Singida ndiye aliyeteuliwa.
Uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Julai 31, 2019 kujaza nafasi iliyoachwa na Tundu Lissu ambapo ilielezwa na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kwamba amepoteza sifa.
Social Plugin