Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Video Mpya ya Gospel : IRENE ROBERT - TEMBEA


Baada ya kukamata anga la Muziki la Injili ndani na nje Tanzania kwa wimbo wake uitwao Kishindo,Msanii wa Muziki wa Injili kutoka Tanzania,Irene Robert, sasa ameachia video Mpya,wimbo unaitwa Tembea. 

'Tembea' ni wimbo wake wa nne kuachia baada ya kushusha wimbo wa kwanza uitwao Unashuka, Nianze na wewe kisha Kishindo


Video ya Tembea imefanywa na Enxer huku audio ikifanyika pale Masai Record chini ya producer Yusuph Manamba ambaye yupo chini ya Lebo ya Famara Promotion.

Irene ni mwimbaji ambaye amepata mafanikio kwa haraka sana kutokana na kufanya kazi nzuri za kiwango cha juu sana aliyejishusha kwa unyenyekevu na anatamani kwenda anga za kimataifa zaidi.

Tumia dakika zako chache kutazama video hii ya Tembea kutoka kwa Msanii Irene Robert hapa chini... Hakika utabarikiwa mtu wangu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com